Kitaifa

Simba Yaanza Mazoezi na Wachezaji Wawili tu

on

TIMU ya Simba imeanza mazoezi hii leo katika uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi utakaoanza mwezi ujao lakini ni wachezaji wawili pekee ndio waliohudhuria.

Viongozi wa klabu hiyo walitoa taarifa wiki kadhaa zilizopita kuwa Julai 5 ambayo ni leo wataanza maandalizi ya msimu ujao na ndicho kilichotokea lakini ni mabeki Jamal Mwambeleko na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ tu ndio waliojitokeza kwenye mazoezi hayo.

Kaimu Makamu wa Rais wa klabu hiyo Idd Kajuna ameithibitisha BOIPLUS kuwa wameanza mazoezi leo huku wakisubiri wachezaji wengine walio katika timu ya Taifa na wale wa kigeni kujiunga kwa ajili ya kuanza kambi ya pamoja ambayo itakuwa ndani ya nchi itakayochagizwa na mechi za kujipima nguvu.

“Timu imeanza mazoezi leo kwenye uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini, tunasubiri wachezaji wote wakamilike ili tuanze kambi,” alisema Kajuna.

Mwarami Mohammed

Wakati huo huo Wekundu hao wamemtangaza Mwarami Mohammed kuwa kocha wa magolikipa akichukua nafasi ya Idd Salum huku pia kocha msaidizi Jackson Mayanja akionyeshwa mlango wa kutokea.

Taarifa ndani ya Simba zinasema kuwa, uongozi umeamua kufanya mabadiliko katika benchi la ufundi kwa ajili ya kuongeza ufanisi huku kocha mkuu Mcameroon Joseph Omog akiendelea kupeta.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *