Kitaifa

Simba,Yanga Wakitisha tu Everton Hii Hapa

on

KLABU ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza itashuka dimbani Julai 13 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya bingwa wa michuano mpya ya SportPesa Super Cup ambayo Simba na Yanga ni timu ambazo zitashiriki.

Everton ambayo inadhaminiwa na kampuni ya SportPesa itakuja chini ikiwa na kikosi kizima kinachonolewa na kocha raia wa Uholanzi Ronald Koeman katika mchezo huo ambao pia wataumia kama maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Robert Elston alisema mchezo huo utatumiwa na kocha wao kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huku akijivunia kuwa timu ya kwanza inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza kucheza na timu kutoka Afrika Mashariki.

“Kocha Ronald Koeman na wachezaji wake watautumia mchezo huo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na pia wanategemea mchezo mzuri,” alisema Elston.

Kwa upande wake Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alisema ujio wa klabu hiyo utakuwa msaada mkubwa kwa klabu za Tanzania kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa Everon.

“Ujio wa Everton nchini utakuwa na faida kubwa kwa timu zetu hapa nchini kwakua zitajifunza moja kwa moja kuhusu masuala mbalimbali ya kiutawala na kiufundi,” alisema Dk Mwakyembe.

Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza Juni 5 katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam ikishirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambazo ni Simba, Yanga, Singida United, Jang’ombe Boys, Nakuru All Stars, Tusker, Gor Mahia na AFC Leopards.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *