Kitaifa

Singida United Nayo Yaingia Anga za Yanga

on

YANGA inadaiwa kuzungumza na kipa wa African Lyon, Youthe Rostand kwa ajili ya kumsajili kwenye kikosi chao cha msimu ujao ingawa hawajamlizana naye lakini Singida United tayari nayo imetia mguu kwa kipa huyo.

Mbali na kuwania saini ya Rostand, Singida United ambao wamepanda kushiriki ligi kuu msimu ujao pia wamefanya mazungumzo ya siri na beki Miraji Adam ambaye pia amemaliza mkataba na Lyon iliyoshuka daraja.

Hivi karibuni Yanga imekuwa ikiporwa wachezaji ambao wamezungumza nao kwa ajili ya kuwasajili akiwemo Waziri Junior, Mbaraka Yusuph na Salmini Hoza ambao wametua Azam FC.

Wachezaji wote hao walikuwemo kwenye mipango ya usajili ya Yanga ambao sasa wanaonekana kuyumba kiuchumi hivyo kupelekea wachezaji wanaowahitaji waishie kusaini kwingine.

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa uongozi wa Singida United unafanya kila mbinu za kuwanasa wachezaji hao wawili na kinachosubiriwa ni kupewa pesa ambayo wameipendekeza.

“Bado wanaendelea na mazungumzo hasa kwa kipa Rostand lakini Miraji walifikia makubaliano ingawa bado hawajamalizana katika kupeana mkataba nadhani kuna mambo wanayaweka sawa,” alisema kiongozi huyo.

Miraji Adam

BOIPLUS ilizungumza na Miraji ambaye alikiri kuwepo kwa mazungumzo hayo na sasa anasubiri viongozi wa Singida United waamue kwani yeye amewapa mapendekezo yao.

“Tulizungumza na viongozi wa Singida na tulifikia makubaliano fulani hivyo nawasubiri wao, mpira ndiyo ajira yangu hivyo popote nacheza ili mradi makubaliano yetu yaende vizuri, maana hata Simba nao walinipigia ila hatukuzungumza hadi mwisho,” alisema Miraji.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *