Kitaifa

Singida United Wamshangaza Miraji Adam

on

BEKI wa zamani wa African Lyon, Miraji Adam amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Singida United wenye thamani ya Sh 20 milioni ambazo amesema hajawahi kuzipata tangu aanze kucheza soka lake.

Usajili huo umefanyika leo Jumatano mchana jijini Dar es Salaam ambapo ametamka kwamba amefanya uamuzi huo kwani anaona Singida United ni sehemu sahihi kwake.

Akizungumza na BOIPLUS, Miraji alisema kuwa miaka yote aliyocheza soka ikiwemo klabu kubwa hapa nchini ya Simba hakuwahi kupewa pesa nyingi kama hiyo zaidi aliishia kukamata Sh 15 milioni ambazo pia alipewa kwa awamu.

Miraji akisaini mkataba wa miaka miwili

“Yaan hapa ni kama naanza kufaidi soka kwani sijawahi kusajiliwa kwa pesa kama hii, nilipewa pesa kidogo ambayo pia ilitolewa kwa mafungu ambapo kufanya jambo lako kwa wakati mmoja ilikuwa ni vigumu.

“Hapa nimelipwa pesa yote ambapo nitaweza kufanya jambo la maana kwa wakati mmoja, naahidi kwamba nitajituma zaidi kuisaidia timu kwani nao wanaonekana wamejipanga hivyo sitawaangusha,” alisema Miraji.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *