Kitaifa

Singida Wamkana Bossou

on

UONGOZI wa klabu ya Singida United umekanusha taarifa za kuhitaji saini ya beki wa kati wa Yanga raia wa Togo Vincent Bossou kutokana na kutohitajika kwa mchezaji wa kimataifa kwa sasa.

Singida tayari imesajili wachezaji sita wa kimataifa wakiwa na nafasi moja ya kuongeza nyota mwingine lakini hakuna nafasi ya beki huyo katika mipango yao ya msimu ujao.

Meneja wa klabu hiyo Festo Sanga amewaambia Waandishi wa Habari kuwa tetesi zinazo wahusisha na kutaka kumsajili beki huyo sio za kweli na amekanusha kwa kusema hakuwa kwenye mipango yao.

“Hatujawahi kumhitaji Bossou hizo mnazozisikia ni tetesi tu. Tumesajili wachezaji 24 tuna nafasi ya kuongeza wengine wanne ila hatuna mpango na Bossou,” alisema Sanga.

Sanga alisema klabu hiyo imefanikiwa kununua basi lenye thamani ya shilingi 350 milioni kwa ajili ya safari mbalimbali za timu wakati wa mashindano.

Wakati huo huo kikosi chao kitaingia kambini kesho jijini Mwanza kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi ambapo wanatarajia kucheza mechi za kirafiki na timu kutoka katika nchi za Kenya, Uganda na Rwanda.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *