Kitaifa

Singida Wamshusha Bongo Mkali wa Mabao Rwanda

on

BAADA ya kimya cha muda mrefu hatimaye timu ya Singida United imerudi tena kwenye soko la usajili na hii leo wamefanikiwa kuipata saini ya mshambuliaji Danny Usengimana anayechezea Polisi FC ya nchini Rwanda.

Tangu ilipopanda Daraja Singida ilifanya usajili wa haraka haraka kabla ya kupunguza kasi na kuacha timu nyingine zinazoshiriki ligi kuendelea kutesa sokoni na leo wamerejea tena kwa kumnasa Mnyarwanda huyo mkali wa mabao.

Danny Usengimana kulia akiichezea timu ya Rwanda

Mshambuliaji huyo ambaye pia anachezea timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavumbi’ ameibuka mfungaji bora mara mbili mfufulizo nchini humo akifunga juma ya mabao 32 kitu ambacho kinaweza kuwa faida kwa Singida msimu ujao.

Nyota huyo mwenye miaka 21 amekabidhiwa jezi 10 kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo iliyopanda daraja baada ya miaka 16.

BOIPLUS ilikuwa ya kwanza kuripoti juu ya usajili wa nyota huyo mara viongozi wa Singida walipoanza naye mazungumzo mapema mwezi Aprili mwaka huu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *