Kitaifa

Singida Wayatema Mamilioni ya SportPesa Mapemaa

on

SINGIDA United imekuwa timu ya kwanza kuaga mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kutolewa kwa mikwaju ya penalti 5-4 na AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Singida walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10 kwa kichwa kupitia kwa Kutinyu Tafadzwa baada ya mabeki wa Leopards kuzembea kuondoa hatari.

Vincent Oburu aliisawazishia Leopards dakika ya 63 kwa shuti la mguu wa kushoto baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Singida.

Nyota wa AFC Leopards wakishangilia baada ya kusawazisha bao

Baada ya bao hilo Leopards waliendelea kulisakama lango la Singida kwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara lakini hawakufanikiwa kupata bao.

Kocha wa Singida Hans Pluijm aliwatoa Mtasa Widson na Kutinyu kisha kuwaingiza Nizar Khalfan pamoja na Yusuph Kagoma mabadiliko ambayo hayakusaidia kitu.

Penati za Leopards zilifungwa na Mangoli Bernad, Marslelas Ingots, Alan Katerega, Duncan Otieno na Fiamenyo Gilbert huku Atupele Green, Hamis Shengo, Moroiwa Elisha na Dumba Hassan wakifunga kwa upande wa Singida na Salum Chuku akikosa mkwaju wake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *