Kitaifa

Soka la Ufukweni Sasa Laelekea kuingia Mtaani

on

MCHAKATO wa kutafuta vipaji vya wachezaji wa soka la ufukweni waliopo mtaani unatarajiwa kuanza kufuatia muda mrefu kutegemea wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali hapa jijini Dar es salaam.

Soka la ufukweni limeanza kupata umaarufu katika miaka ya karibuni nchini baada ya timu  ya Taifa ya mchezo huo kushiriki michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi japokuwa bado haijaanza kufanya vizuri.

Akizungumza na BOIPLUS kocha wa timu ya Taifa ya mchezo huo John Mwansasu amesema tarehe rasmi ya kuanza zoezi hilo haijapangwa kutokana na kukosekana kwa wadhamini wa kuendesha programu hiyo kwa sasa.

Mwansasu alisema wataendelea kutegemea wanafunzi wa vyuo japokuwa muda mwingi wanakuwa kwenye masomo hivyo kupelekea kuwakosa hususani katika maandalizi ya mashindano ya kimataifa.

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya soka la ufukweni, John Mwansasu

“Programu ya kutafuta wachezaji mtaani bado haijaanza, tunaongea na wadhamini kwa ajili ya kuendesha zoezi hili kwa ngazi za klabu kutoka hapa jijini Dar es salaam,” alisema Mwansasu.

Ameongeza kuwa program hiyo ina lengo la kusaka wachezaji watakaounda timu ya taifa ambapo pia wanatarajia kuwafikia wachezaji kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao watakuwa msaada kwa Taifa katika siku za usoni.

“Mchezo huu unahitaji rasilimali fedha kwa ajili ya maandalizi na kuusambaza sehemu mbalimbali nchini kwakua bado haujafahamika vizuri,” alisema Mwansasu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About William Kange

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *