Kitaifa

Soma Mkwara wa Beki wa Toto Aliyetua Msimbazi

on

Akram Msangi, Dar

BEKI mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Toto African ya jijini Mwanza, Yusuph Mpili amesema amejiunga na mabingwa hao wa Kombe la FA ili kupata nafasi ya kucheza na sio kukaa benchi.

Yusuph aliyesaini mkataba wa miaka miwili na Wekundu hao jana ameweka wazi kuwa viongozi wa klabu hiyo walimfuata kabla ya kukutana kwenye mchezo wa marudiano wa ligi na kukubaliana kukamilisha dili ligi itakapomaliza.

Beki huyo ameiambia BOIPLUS kuwa, “Nimesaini miaka miwili na Simba na nipo kwa ajili ya kucheza na sio kukaa benchi. Mwalimu akinipa nafasi nina imani nitatoa mchango mkubwa kwa timu,”.

Mpili tayari yupo kambini na Wekundu hao kujiwinda na michuano mipya ya SportPesa Super Cup inayoshirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya itakayoanza Juni 5 kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Beki huyo pamoja na nyota wengine wapya kama Jamal Mwambeleko toka Mbao FC na Ahmed Msumi (Ndanda) wataonekana wakiwa na jezi nyekundu kwa mara ya kwanza katika mchezo dhidi ya Nakuru All Stars Juni 6.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *