Kitaifa

Stars ‘Dozi’ Mara Mbili Misri, Lesotho Wajipange

on

ALEXANDRIA, Misri
TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambayo ipo nchini Misri kwa kambi ya wiki mbili itaanza kufanya mazoezi mara mbili kwa siku ‘dozi kutwa mara mbili’ kuivutia kasi Lesotho kwa ajili ya mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwezi Juni.

Stars ambayo itarejea nchini Juni 7 itashuka dimbani siku tatu baadae kucheza na Lesotho kwenye uwanja wa Azam Complex mtanange utakaonza saa 2 usiku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kutoka mjini Alexandria nchini Misri inasema kuwa kocha mkuu wa Stars Salum Mayanga ataanza programu ya mazoezi saa 2 usiku wa leo ambapo kuanzia kesho itakuwa ni asubuhi na usiku.

Makocha wa Stars wakikagua viwanja kwa ajili ya kufanyia mazoezi

Mayanga alisema pia keshokutwa Ijumaa watakuwa na programu ya darasani asubuhi kabla ya usiku kuendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kurejea nchini tayari kwa mchezo huo.

“Programu ya mazoezi kwa timu itaanza leo saa 2.00 usiku lakini kuanzia kesho tutakuwa na vipindi viwili vya mazoezi asubuhi na usiku na Ijumaa tutaanza na programu ya darasani na usiku itakuwa uwanjani kama kawaida,” alisema Mayanga.

Timu za Uganda na Cape Verde pia zipo kundi L pamoja na Stars na Lesotho ambazo zitaumana Juni 11.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *