Kitaifa

Stars Yaendelea Kuliamsha Dude Sauzi, Leo Yawatuliza Wenyeji

on

RUSTENBURG, Afrika Kusini
TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetinga nusu fainali ya michuano ya COSAFA baada ya kuwatoa wenyeji Afrika Kusini kwa bao moja katika mchezo wa robo fainali na sasa itakutana na Zambia.

Stars ambayo ni timu mwalika kutokana na kutokuwa mwanachama wa COSAFA ilikuwa kinara wa kundi A baada ya kufikisha pointi tano zilizowafikisha katika hatua hiyo.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji Elius Maguri dakika ya 17 baada ya kupokea pasi safi ya Mzamiru Yassin kutoka katikati ya uwanja.

Wenyeji walimiliki sehemu kubwa ya mchezo huo kwa kuliandama lango Stars lakini safu ya Ulinzi iliyokuwa ikiongozwa na Erasto Nyoni na Salim Mbonde ilikuwa imara licha ya makosa machache ambayo yangeweza kuigharimu timu.

Maguri alichaguliwa mchezaji bora wa mechi hiyo na kufanya kuwa mchezaji wa nne kutoka Tanzania kupata tuzo katika mashindano hayo.

Wengine waliopata tuzo ya mchezaji bora wa mechi kutoka Tanzania ni Shiza Kichuya, Mzamiru na Nyoni.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *