The sports Hub

Straika Mwadui aitamani Stars

0 15

MCHANA nyavu  wa Mwadui FC, Salim Aiyee amesema ndoto yake kubwa ni kuiwakilisha Tanzania kimataifa kupitia timu ya Taifa, (Taifa Stars).

Straika huyo mwenye mabao 16 kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ‘TPL,’ amesema anatami siku moja kuwa mmoja kati ya wachezaji watakao peperusha bendera ya Tanzania vizuri katika mashindano mbalimbali ambayo timu hiyo itakuwa inashiriki.

“Ndoto yangu kubwa siku moja kuiwakilisha nchi yangu katika mataifa mbalimbali kwasasa najituma kwa nguvu zangu zote ili kuwaonyesha walimu wa timu ya taifa uwezo nilio nao, naamini ipo siku ndoto zangu zitakua kweli,” amesema mshambuliaji huyo.

Aidha Aiyee ameweka wazi kuvutiwa na mchezaji

wa kimataifa anaekipiga nchini Ubelgiji katika timu ya KRC Genk, Mbwana Samatta na kusema anatamani siku moja kuja kuwa kama yeye.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.