Kitaifa

Taifa ilikuwa ni Rooney tu

on

KIVUTIO pekee kwa wadau wa soka waliofurika uwanjani kushuhudia mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Everton na Gor Mahia ni mshambuliaji Wayne Rooney aliyesajiliwa akitokea Manchester United hivi karibuni.

Wengi walitaka kushuhudia ubora wa mwanasoka huyo ambaye alifunga bao la kwanza dakika ya 34 ikiwa ni bao lake la kwanza tangu kusajiliwa na klabu yake hiyo ya zamani.

Mechi hiyo iliyoratibiwa na Kampuni ya michezo ya kubashiri imechezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Everton imeibuka na ushindi wa bao 2-1.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Uingereza alifunga bao hilo maridadi kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa Gor Mahia, Boniface Oluochi.

Dakika ya 20 ya mchezo huo shabiki aliyefahamika kwa jina la Hans Hassan alikimbia na kufanikiwa kuingia uwanjani na kumkumbatia Rooney.

Kinyume na matarajio ya mashabiki wengi walijitokeza kwenye mchezo huo Gor walikuwa imara zaidi na kufika mara nyingi langoni mwa Everton ambapo walisawazisha dakika ya 37 kupitia kwa mshambuliaji Jacquer Tuyisenge kwa kichwa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Karim Nizigiyimana.

Kocha wa Everton Mholanzi Ronald Koeman aliwatoa wachezaji wote walioanza kipindi cha kwanza ambao waliongeza kasi na kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Kierdin Dowell kwa shuti kali nje ya 18 dakika ya 81.

Kwa upande wake kocha Dylan Kerr wa Gor aliwatoa Oluocha, Medie Kagere, Karim, Tuyisenge, Mussa Mohammed, Kennedy Muguna na kuwaingiza Frederick Odhimbo, Ochieng Wellington, Jean Mugiraneza, Innocent Wafulla na Simiyu Mike.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *