Kitaifa

Hizi hapa sababu za TAKUKURU Mwanza kuwashikilia akina Dauda

on

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Mwanza iliwashikilia kwa muda viongozi wa soka kutokana na viashiria vya rushwa na kuanza kampeni kabla ya muda kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF mwezi ujao.

Viongozi walioshikiliwa ni Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almas Kasongo na mjumbe wake Shaffih Dauda, Katibu wa chama cha soka Mkoa wa Mwanza Elius Mwanjali, Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mbeya na wajumbe wa mikoa ya jirani.

Meneja wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza, Ernest Makele amethibitisha kuwashikilia viongozi hao toka usiku wa jana lakini waliachiwa kwa dhamana huku uchunguzi dhidi yao ukiendelea.

Safu ya uongozi wa DRFA ambapo mwenyekiti Almas Kasongo na mjumbe Shaffih Dauda ni katika walioshikiliwa na TAKUKURU jijini Mwanza

Viongozi hao walikuwa katika
kuhamasisha michuano ya Ndondo Cup mkoani humo usiku wa jana lakini taasisi hiyo iliwatilia shaka kabla ya kuwashikilia kwa muda na kuachia kwa dhamana huku uchunguzi juu yao ukiendelea.

Dauda ni mmoja wa wagombea katika nafasi ya ujumbe wa Kamati ya utendaji kanda ya Dar es Salaam katika uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12.

Kampeni za uchaguzi huo zitaanza Agosti 5 kwa wagombea wa nafasi zote.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *