Kimataifa

Terry Kukamata Mikoba Aston Villa

on

BIRMINGHAM, Uingereza
KLABU ya Aston Villa imefanikiwa kumsajili nahodha wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza John Terry ambaye ameruhusiwa kutimka darajani hapo.

Mkataba wa Terry 36, katika viunga vya Stamford Bridge ulimalizika Juni 30 ambapo sasa amesaini mwaka mmoja na timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza ‘Championship’.

Terry, ameshinda mataji 78, na ameicheza Chelsea mechi 717 na kutwaa mataji matano ya ligi kuu ya Uingereza.

Villa ilimaliza nafasi ya 13 katika ligi daraja la kwanza msimu uliopita ambapo kocha Steve Bruce amepanga kuhakikisha anamaliza nafasi za juu msimu wa 2017/18.

Meneja wa Birmingham City Harry Redknapp alisema mapema mwezi Juni kuwa alipeleka ofa kwa ajili ya Terry baada ya kutangaza mwezi Aprili kwamba ataikacha Chelsea.

Terry amechezea timu mbili pekee nchini Uingereza ambazo ni Chelsea na Nottingham Forest ambayo alichezea kwa mkopo wa muda mfupi mwaka 2000.

“Ni klabu kubwa ambayo nilikuwa naipenda toka zamani,” Terry aliuambia mtandao wa Aston Villa.

“Kuna vifaa vizuri vya mazoezi na afya, uwanja wa Villa Park ni miongoni mwa viwanja bora katika nchi hii, kuna wachezaji wazuri wenye uzoefu na meneja Steve Bruce namkubali pia.

“Nasubiri kuanza msimu mpya nijiunge na wachezaji wenzangu nadhani naweza nikasaidia na kuwa na msimu mzuri wa ligi.”

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *