Kimataifa

Tetesi na Habari za Usajili Barani Ulaya

on

LIVERPOOL KUMNYAKUA CLICHY BURE

Liverpool wamempa mkataba wa miaka miwili beki wa kushoto wa Manchester City Gael Clichy ambaye amemaliza mkataba wake na vijana hao wa kocha Pep Guardiola.

Clichy ni miongoni mwa nyota kadhaa wa City ambao ‘wamepigwa panga’ na Guardiola ambaye anataka kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya michuano mbalimbali barani Ulaya.

Kocha wa Liverpool Jurgen Kloop anataka kuimarisha kikosi chake ambapo pia anahusishwa na kumnyakua kiungo mshambuliaji wa AS Roma Mohammed Salah kwa ada ya pauni 43 milioni.

ARSENAL YAMNASA KINDA KUTOKA UBELGIJI

Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano ya ada ya uhamisho wa pauni 6.8 milioni kwa mshambuliaji Henry Onyekuru raia wa Nigeria anayechezea timu KAS Eupen ya Ubelgiji.

Washika bunduki hao wa London wamekuwa na mazungumzo na timu hiyo ya Ubelgiji toka wiki iliyopita ambapo sasa wamefanikiwa kupata saini ya nyota huyo mwenye miaka 19.

UNITED WANA UHAKIKA WA KUBAKI NA DE GEA WAO

Klabu ya Manchester United ina uhakika wa kumbakisha mlinda mlango wake David De Gea katika majira haya ya joto licha ya kuonyesha nia ya kutaka kujiunga na Real Madrid.

De Gea alikaribia kujiunga na Real katika majira ya joto mwaka 2015 ambapo miamba hiyo ya Hispania imeendelea kuhitaji saini yake hadi leo.

Vyanzo vya habari kutoka Uingereza vinasema kuwa De Gea ana furaha na maisha ndani ya United chini ya kocha Jose Mourinho pia kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao .

Mlinda mlango huyo namba moja wa timu ya taifa ya Hispania amebakisha miaka miwili na United ambapo kuna kipengele cha kumruhusu kuongeza mwaka mmoja tena.

 

KIPA WA PSG KUMRITHI BEGOVIC CHELSEA

Asmir Begovic

mabingwa wapya wa ligi kuu nchini Uingereza timu ya Chelsea inataka kumsajili mlinda mlango wa PSG Alphonse Areola kuchukua nafasi ya Asmir Begovic aliyetimkia Bournemouth.

Areola 24, amecheza michezo 15 msimu uliopita na anaamini ni muda muafaka kwake kupata changamoto mpya kutoka kwa Thibaut Courtois ndani ya Chelsea.

Sababu ya Begovic kuondoka klabuni hapo ni kukosa nafasi ya kucheza kwani kocha Antonio Conte amekuwa akimuamini zaidi Courtois kusimama langoni.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *