The sports Hub

Tetesi za Usajili Barani Ulaya Jumatatu Novemba 26

0 173
Eliaquim Mangala (kushoto)

Inter Milan na Wolves wameonyesha nia ya kumsajili mlinzi wa kati wa Manchester City, Eliaquim Mangala kwa uhamisho huru katika dirisha lijalo la majira ya joto (Source: Sun on Sunday)

 

Eden Hazard

Chelsea ni kama vile hawana tena cha kufanya juu ya kumpoteza nyota wao Eden Hazard huku Real Madrid wakionekana kuwa mstari wa mbele katika kuwania saini yake. (Source: OK Diario)

 

Cesc Fabregas

Cesc Fàbregas amewayavutia macho ya ‘Wanene’ wa Beşiktaş ya Uturuki lakini AC Milan wanabaki kuwa wenye nafasi kubwa zaidi ya kumsainisha kiungo huyo wa Chelsea. (Source: Sunday Express)

 

Kocha wa Manchester United, José Mourinho anaweza kupewa wachezaji wawili wa Inter Milan, Milan Škriniar na Ivan Perišić kama atakuwa tayari kumuachia Paul Pogba aelekee kwenye jiji la Milan. (Source: Daily Star)

 

Juan Mata

Manchester United wanajiandaa kumpatia Juan Mata mkataba wa miaka mitatu baada ya Arsenal na Atlético Madrid kuweka mitego ya kumnasa Mhispaniola huyo akiwa huru katika dirisha lijalo la majira ya joto. (Source: Sunday People)

 

Neymar na Mbappe

PSG wapo tayari kumuuza Neymar na kujenga timu yao kupitia kwa kinda Kylian Mbappé kwa lengo la kukwepa vikwazo vya mizania ya kifedha (Financial Fair Play). (Source: Mail on Sunday)

 

 

OFFICIAL | Nyota wa Atlético Madrid, Antoine Griezmann na Lucas Hernandez wamesaini mikataba ya miaka mitano na sita kwa mfuatano. (Source: @Atleti)

Get real time updates directly on you device, subscribe now.