The sports Hub

Tetesi za usajili barani Ulaya

0 14

‘Wanene’ Madrid Wamtaka Mourinho Bernabeu

Kocha Julen Lopetegui amekuwa katika wakati mgumu kufuatia matokeo mabovu ya Real Madrid tangu ajiunge nayo huku wachambuzi wa masuala ya soka wakimtabiria kutodumu klabuni hapo.

Katika kile kinachoonekana kuwa safari ya kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania ni fupi klabuni hapo, kuna taarifa zinadai kuwa bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo inataka Jose Mourinho atue Santiago Bernabeu kuchukua mikoba ya Lopetegui. (SOURCE: El Chiringuito)

Safari ya Sterling Yanukia City
Manchester City wameshindwa kukubaliana na mahitaji ya Raheem Sterling kwa ajili ya mkataba mpya ambapo nyota huyo anataka alipwe paundi 300,000 kwa wiki.

Jambo hilo linachochea hofu kwamba winga huyo wa timu ya taifa ya Uingereza anaweza kutimka klabuni hapo katika dirisha lijalo la majira ya joto. (SOURCE: Daily Mirror)

Raheem Sterling

Arsenal ‘Wanajiuliza’ Kuhusu Winga wa Barcelona
Klabu ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kumpata kwa mkopo winga wa Barcelona ya Hispania, Malcom ili aweze kuimarisha zaidi kikosi hicho. (SOURCE: Sport)

Mourinho Awapanga Mabosi Wake United
Wakati watu wengi wanafikiria kocha Jose Mourinho wa United atatimuliwa kazi, mwenyewe yupo ‘busy’ na mipango ya kukiimarisha kikosi chake.

Kocha huyo amewaomba mabosi wake waandae ‘fungu’ kwa ajili ya kumtwaa beki wa Napoli raia wa Senegal, Kalidou Koulibaly Januari 2019. (SOURCE: Daily Mirror)

 

Marcelo

Marcelo Kumfuata Ronaldo?
Mtandao wa Tuttosport umeripoti kuwa beki wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo ameiambia klabu hiyo kuwa anataka kujiunga na Juventus ya nchini Italia.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.