Kitaifa

TFF yazipiga Mkwara timu za ligi kuu

on

SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeziambia klabu zinazoshiriki ligi kuu halitaongeza muda wa usajili na timu isipokamilisha idadi ya wachezaji 18 wa ndani itashushwa daraja.

Dirisha la usajili lilifunguliwa Juni 15 na litafungwa Agosti 6 ambapo TFF imezikumbusha klabu kukamilisha taratibu zote mapema kabla ya tarehe tajwa ili kuepuka rungu la kushushwa daraja.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema msimu uliopita kuna timu zilichelewa kukamilisha usajili wakiwemo mabingwa watetezi Yanga kitu ambacho hakitatokea msimu huu.

“Nichukue nafasi kuzikumbusha klabu kukamilisha usajili kwa wakati kwakua hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe iliyopangwa kupita.”

“Kwa mujibu wa kanuni timu zinazoshiriki ligi lazima wasajili wachezaji 18 wazawa ambao taratibu zake lazima zifuatwe ikishindikana hapo, timu husika itashushwa daraja,” alisema Lucas.

Lucas amezitaka timu hizo kuzingatia mikataba ya wachezaji katika kipindi hiki cha usajili ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *