The sports Hub

TIGO FIESTA DAR: Wasanii Watakaopanda ni Kama ‘Chips Zege’

0 675

WAANDAJI wa Tamasha la Tigo Fiesta 2018 kampuni ya Clouds Media Group (CMG) wametangaza majina 28 ya wasanii wanaotarajia kupanda jukwaani Jumamosi hii katika ile inayofahamika kama Grand Finale kwenye viwanja vya Leaders Club.

Orodha hiyo iliyotangazwa asubuhi ya leo inajumuisha wasanii waliong’ara miaka ya hivi karibuni pamoja na wakongwe jambo linaloashiria kutakuwa na mchanganyiko wa kipekee na kutoa kitu chenye kuvutia mfano wa ‘chips zege’.

Hii ndio hali ilivyo kwenye viwanja vya Leaders Club hadi sasa.

Hii hapa orodha kamili ambayo inaelezwa pia kuwa idadi itaongezeka.

1. Weusi
2. Rostam
3. Fid Q
4. Wakazi
5. Rich Mavoco
6. The Mafik
7. Ben pol
8. Rosa Ree
9. Marioo
10. Barnaba
11. Billnass
12. Chege Chigunda
13. Dogo Janja
14. Msami
15. WhoZu
16. Mimi Mars
17. Lulu Diva
18. Zaiid
19. Mesen Selekta
20. Maua Sama
21. Tid
22. Qchief
23. Juma Nature
24.Jolie
25.Benson
26.Jay Melody
27.Mabantu
28.Brian Simba

Hata hivyo, waandaji hao wamesema kuna orodha ya nyingine inayofahamika kama Kambi Rasmi ya Upinzani itatangazwa baadaye.

Kiingilio katika tamasha hilo kimepangwa kuwa ni sh. 10,000 ukinunua kwa Tigopesa master-pass QR na sh. 15,000 ukinunua kawaida.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.