The sports Hub

TINO: Warembo Wananogesha Filamu Bwana

0 46

MWIGIZAJI wa filamu nchini, Hisani Muya ‘Tino,’ ameweka wazi kuwa sababu kubwa inayofanya filamu za mapenzi kuuza zaidi ni uwepo wa warembo.

Tino alisema kwamba warembo hao pamoja na kuzifanya filamu zivutie pia huwa na juhudi katika kazi hiyo tofauti na wanaume. Alisema wasichana warembo wanatumika katika filamu kwa kuwa pia wana juhudi za kufanya mambo tofauti kila siku na wanaipenda kazi yao.

“Kwa kweli bila kuweka wasichana warembo katika filamu yako hutauza kwa sababu wengi wana juhudi za kufanya mambo mapya kila kukicha, lakini pia wanakuongezea mvuto kwa kuwa warembo ni kama maua,” alisema Tino.

Aliongeza kuwa mizengwe wanayokutana nayo ni kutokana na umaarufu wao lakini kama binadamu wanahitaji faragha ya kuwa na maisha yao nje ya kazi kitu ambacho wanakikosa kutokana na kuwa maarufu.

Tino aliongeza kuwa lawama zimekuwa nyingi lakini na mafanikio yanaonekana kwani kwa sasa wasichana hao ndio wanaomiliki ‘mijengo’ mikali hapa mjini pamoja na kuishi vizuri.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.