Kitaifa

Tisa tu wabaki, 16 wapya Singida United yafunga usajili

on

SINGIDA United imefunga usajili kwa kusajili nyota 16 wapya huku wakiwabakiza wachezaji tisa pekee walioipandisha daraja timu hiyo kushiriki msimu mpya wa ligi kuu unaotarajia kuanza mwezi ujao.

Hiyo ina maana kwamba Singida United imesajili kikosi kizima cha kwanza ambacho kitakuwa kipya na leo wamefunga usajili wao kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili nahodha wa Ndanda FC, Kigi Makasi.

Singida United inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans Pluijm imesajili nyota saba wa kigeni ambao ni Elisha Muroiwa, Twafadzwa Kutinyu, Simbarashe Nhivi, Wisdom Mtasa, Shafik Batambuze, Dany Usengimana na Michel Rusheshangoga.

Nyota wapya wazawa ni Atupele Green, Miraj Adamu, Kenny Ally, Roland Msonjo, Pastory Athanas, Deus Kaseke, Ally Mustapha na Makasi.

Uongozi wa klabu hiyo pia umewatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji wao waliokuwa na mikataba na timu hiyo ambao waliipandisha daraja.

Singida United kwa sasa ipo jijini mwanza ambako imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya ligi huku ikicheza mechi mbalimbali za kirafiki ili kumpa nafasi kocha kuona mapungufu ya kikosi chake.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *