Kitaifa

Try Again, Kajuna Wakabidhiwa Mikoba ya Aveva, Kaburu Simba

on

Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Simba imemteua mjumbe Salim Abdallah ‘Try Again’ kukaimu nafasi ya Rais huku Iddy Kajuna akiwa msaidizi wake.

Wajumbe hao wameteuliwa katika kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Jana jijini Dar es Salaam.

Try Again anakaimu nafasi ya Evans Aveva wakati Kajuna anashika madaraka ya Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambao wanashikiliwa na vyombo vya dola kwa tuhuma za kughushi nyaraka za klabu pamoja na kutakatisha pesa.

Wajumbe hao wataendesha shughuli za klabu hadi hapo ambapo dola itawaachia huru watuhumiwa hao ambao wapo rumande katika gereza la Keko.

Kaimu Katibu mkuu wa Simba, Hamis Kisiwa amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu katika kipindi hiki cha mpito.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *