Kitaifa

Tshabalala Amaliza Msimu kwa Kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora

on

BEKI wa kushoto timu ya Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amekuwa mchezaji wa mwisho kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi msimu huu kufuatia kuibuka kinara wa ligi kuu ya Vodacom kwa mwezi Mei.

Tshabalala amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha kocha Joseph Omog kwa kucheza mechi zote huku akiwashinda Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC katika kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Mei kulikuwa na mechi tatu ambazo nyota huyo alicheza kwa dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kupata matokeo licha ya kumaliza nafasi ya pili mpaka ligi inamalizika.

Pia beki huyo alionyesha nidhamu ya hali ya juu katika michezo hiyo hali iliyopelekea kutoonyeshwa kadi yoyote.

Kwa kushinda tuzo hiyo beki huyo atapewa kitita cha shilingi 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.

Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mchezaji bora wa mwezi tangu kuanza kwa msimu huu wa 2016/17 ni John Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa Ndanda (Novemba).

Wengine ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma Kaseja wa Kagera Sugar (Januari), Hassan Kabunda wa Mwadui (Februari), Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting (Aprili).

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *