Kitaifa

UCHAGUZI TFF: Madega, Malinzi ‘Wakiwasha’ Urais

on

MBIO za uchaguzi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) zimeanza kwa kasi baada ya wagombea 13 kujitokeza kuchukua fomu katika siku ya kwanza tu iliyopangwa kwa ajili ya zoezi.

Mwamko wa uchukuaji wa fomu umekuwa mkubwa ambapo katika kila nafasi tayari watu wawili au zaidi wameshachukua fomu.

Rais anayemaliza muda wake Jamal Malinzi tayari amechukua fomu huku Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga Iman Madega nae akijitokeza kuchukua fomu kwenye nafasi hiyo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi

Katika nafasi ya Makamu wa Rais Michael Wambura na Mulamu Ng’ambi ndiyo waliojitokeza mpaka sasa kuwania nafasi hiyo.

Katika upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochukua fomu ni Salum Chano, Ephraim Magige, Elius Mwanjala, Golden Sanga, Mbasha Matutu, Shaffih Dauda, Dustan Nkundi na Samwel Daniel.

Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema fomu pia zinapatikana kupitia tovuti ya Shirikisho hilo kwa ajili ya kuwawezesha watu walio mbali kupata nafasi bila kufika jijini Dar es Salaam.

“Zoezi la kuchukua fomu kwa wagombea limeanza leo na tayari watu 13 wamejitokeza katika nafasi mbalimbali. Fomu hizo pia zinapatikana kwenye tovuti ya TFF,” alisema Lucas.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *