Kimataifa

Ujumbe wa Pele kwa Neymar

on

RIO DE JENEIRO, Brazil
GWIJI wa soka nchini Brazil Pele amempongeza Neymar kwa kujiunga na timu ya Paris Saint Germain akitokea Barcelona kwa ada ya pauni 197 milioni.

Mshambuliaji huyo aliyewika akiwa na jezi namba 10 ya timu ya Taifa ya Brazil aliandika;

“Kila la kheri katika changamoto mpya”.

“Paris ni mji mzuri, ni miongoni mwa miji ninayoipenda ,” aliandika mshindi huyo mara tatu wa kombe la dunia kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Neymar amesaini mkataba wa miaka mitano na PSG jana Alhamisi kwa dau hilo lililovunja rekodi ya dunia.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *