Afrika

Ulimwengu afanyiwa upasuaji wa goti Sauzi

on

CAPE TOWN, Afrika Kusini
MSHAMBULIAJI Thomas Ulimwengu atakuwa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa kufuatia kufanyiwa upasuaji wa goti hii leo katika Kituo cha Sayansi ya Michezo cha South Africa Science Sports Center kilichopo Cape Town nchini Afrika Kusini.

Ulimwengu anayechezea klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden alikumbwa na marejuhi hivi karibu kitu ambacho kilimfanya kushindwa kuonyesha uwezo wake katika michezo ya siku za karibuni.

Mchezaji huyo wa zamani wa TP Mazembe ya DR Congo amejiunga na timu hiyo mwezi Januari mwaka huu huku kikosi hicho kilichopanda daraja msimu uliopita kikimuhitaji straika huyo ili awasaidie kujinusuru na janga la kushuka daraja.

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga alimjumuisha Ulimwengu katika kikosi kilichoshiriki michuano ya COSAFA iliyofanyika Afrika Kusini ambayo Stars ilimaliza nafasi ya tatu.

Ulimwengu anatarajiwa kuwepo ‘Sauzi’ kwa wiki mbili zaidi kwa ajili ya mazoezi tiba kabla ya kurejea nchini kuendelea kuuguza jeraha lake.

Hizi hapa ni picha za Ulimwengu kabla hajaondoka hospitalini hapo;

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *