Kimataifa

Umesikia Mkwara wa Wenger Baada ya Kupewa Mkataba?

on

LONDON, Uingereza
BAADA ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amepanga kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza msimu ujao.

Makubaliano ya mkataba huo hayaruhusu mmoja kati ya Wenger na Arsenal kuuvunja ambapo ni lazima Mfaransa huyo afikishe miaka 23 ya kuwanoa Washika Bunduki hao.

Sio Arsenal wala Wenger, 67, ambaye ametanabaisha kuwa huo utakuwa ni mkataba wa mwisho.

“Naipenda sana hii klabu nangalia mbele nione jinsi ya kuisaidia kutwaa mataji,” alisema Wenger baada ya kusaini mkataba huo.

Arsenal wanategemea kutumia pauni 100 milioni kufanya usajili katika dirisha la majira ya joto litakalofunguliwa Julai mosi kiasi kinachokaribiana na walichotumia msimu uliopita.

“Timu yetu ina kikosi imara na tukiongeza nyota wengine kwenye dirisha la usajili tutakuwa bora zaidi.

“Tumejipanga kuleta changamoto kwenye ligi msimu ujao na tutaanzia kwenye usajili,” Wenger aliiambia tovuti ya klabu hiyo.

Wakali hao wa London wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya tano ambayo ni mara ya kwanza tangu Wenger alipoanza kuifundisha mwaka 1996.

Walimaliza pointi 18 nyuma ya vinara Chelsea ambao waliwafunga kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA kwa mabao 2-1 Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Wembley.

Wenger alikutana na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke Jumatatu na kufikia maamuzi ambayo yalipitishwa jana kwenye kikao cha bodi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *