The sports Hub

Unashangaa Viporo vya Yanga?, Nenda Misri ‘Mtu’ Ana Mechi Tisa Mkononi

0 228

UKIUTAZAMA msimamo wa Ligi Kuu nchini Misri kwa sasa kwanza kabisa kama mtanzania utasikitika kuona timu anayochezea Himid Mao, Petrojet FC ikiburuza mkia lakini juu yake kidogo utaona ajabu la mwaka, kuna timu ina viporo nane mwanangu.

Si Ulistaajabu ya Mussa?, Sasa Tazama ya Firauni
Wakati Petrojet ikiburuza mkia kwa kumiliki pointi 11 tu baada ya kushuka dimbani mara 13, juu yake kuna Al Ahly ambayo inashika nafasi ya 17 lakini yenyewe ikiwa imecheza mechi sita tu ambazo ni saba pungufu ya walizocheza Petrojet huku timu kadhaa zikiwa zimeshacheza mechi 14 na moja imepiga mechi 15, habari ndiyo hiyo.

Kwa kifupi hapa ni kwamba wakati tunakerwa na viporo vya waliokuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa na ambao wanazidiwa mechi nne tu na timu zilizocheza mechi nyingi, Yanga, tunapaswa kujiuliza hawa ndugu zetu waarabu wanajisikiaje kuona timu moja ina mechi tisa mkononi?

Kwani Tatizo ni Nini?
Hakuna tatizo, chama cha soka nchini humo (EFA) kwa nyakati tofauti kiliamua tu kuahirisha michezo kadhaa ya timu hiyo ili kuipa nafasi ya kushiriki kikamilifu Ligi ya Mabingwa barani Afrika ambayo walifika hatua ya fainali kabla ya kufungwa na ES Tunis kwa jumla ya mabao 4-3 na wababe hao wa Tunisia kutwaa ubingwa huo.

EFA iliibeba pia Al Masry ambayo ilikuwa ikishiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika kabla ya kuondolewa katika hatua ya nusu fainali na AS Vita ya DR Congo kwa kubamizwa jumla ya mabao 4-0.

Al Masry wenyewe wapo katika nafasi ya 15 baada ya kushuka dimbani mara tisa na kujikusanyia pointi 12 hivyo wanatakiwa kucheza mechi sita zaidi ili kuifikia Al Ittihad iliyocheza mechi 15.

 

MSIMAMO WA LIGI KUU NCHINI MISRI

 

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA

Get real time updates directly on you device, subscribe now.