Kitaifa

Unataka Kugombea Uongozi TFF?, Soma Hapa

on

BAADA ya kutangazwa kwa tarehe rasmi ya uchaguzi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) vigezo vimetolewa kwa wenye nia ya kutaka kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Shirikisho hilo.

Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma ambapo nafasi tatu zitagombewa ambazo ni Rais, Makamu wa Rais na Wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji.

Zoezi la kuchukua fomu na kuzirejesha litakuwa ni kuanzia Juni 16 mpaka 20 na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21 mpaka 23.

Baada ya taratibu zote kufuatwa kampeni kwa wagombea wote zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata uchaguzi huo utafanyika.

Gharama za kuchukua fomu ni kama ifuatavyo; Rais Shilingi laki tano (500,000), Makamu shilingi laki tatu (300,000) na Wajumbe ni shilingi laki mbili (200,000).

SIFA ZA WAGOMBEA.

1-Awe raia wa Tanzania.
2-Awe na kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne (Cheti cha Elimu ya Sekondari).
3-Awe na uzoefu wa uendeshaji mpira wa miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano.
4-Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na asiwe amewahi kuhukumiwa kifungo kisicho na mbadala wa faini.
5-Awe na umri angalau miaka 25.
6-Awe amewahi kuwa ama Mwanasoka, Kocha, Mwamuzi. Au kushiriki katika uendeshaji wa mpira wa miguu angalau katika ngazi ya Mkoa au daraja la kwanza.
7-Awe muadilifu na muaminifu mwenye uwezo wa utendaji katika utekelezaji na utimizaji wa majukumu na malengo ya TFF.
8-Anayegombea nafasi ya Rais au makamu wa Rais awe na kiwango cha elimu kisichopungua shahada moja, mwenye utu na uwezo wa kuiwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *