Kimataifa

United Yamzuia Lukaku Kutua Bongo

on

MANCHESTER, Uingereza
WAPENZI na mashabiki wa soka nchini huenda wakashindwa kumshuhudia mshambuliaji Romelu Lukaku baada ya klabu ya Manchester United kukubali kutoa dau la pauni 75 milioni kwa Everton ambapo dili hilo linategemewa kukamilika muda wowote kuanzia sasa.

Everton wanatarajia kuja nchini kucheza na Gor Mahia Julai 13 ambapo mashabiki wa Tanzania walitarajia kumuona raia huyo wa Ubelgiji lakini taarifa iliyotoka muda mfupi uliopita ni kuwa mshambuliaji huyo hatokuwepo kwenye kikosi cha kocha Ronald Koeman kitakachokuja nchini.

Mbelgiji huyo 24, amefunga mabao 25 katika ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita jambo lilowasukuma United kumfukuzia kwa nguvu zaidi kuashiria dili la mshambuliaji Alvaro Morata limekufa rasmi.

Wayne Rooney

Usajili wa Lukaku hauna uhusiano wowote na nahodha wa United Wayne Rooney kuhamia Everton klabu iliyomlea akiwa mtoto.

Kocha Jose Mourinho anatarajia kukamilisha usajili wa Lukaku kabla ya kikosi chake kwenda Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi Jumapili ijayo.

Mshambuliaji huyo alikuwepo kwenye orodha ya majina ambayo kocha Mourinho alimpa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Ed Woodward kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita.

Mourinho ndiye alimuuza Lukaku Everton kwa ada ya pauni 28 milioni wakati akiwa kocha wa Chelsea mwaka 2014.

Lukaku ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo chini ya wakala Mino Raiola, ambaye alifanikisha United kuwasajili nyota Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan msimu uliopita.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *