Kimataifa

United yaanza kula ‘faida’ kwa Lukaku

on

LOS ANGELES, Marekani
KLABU ya Manchester United imeanza kuonja faida ya kutoa kiasi kikubwa cha pesa kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku baada ya kuanza kuonyesha cheche zake uwanjani katika mchezo wake wa kwanza tu tangu ajiunge nao.

Lukaku amefunga bao lake la kwanza akiwa na United katika ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa maandalizi ya ligi dhidi ya Real Salt Lake alfajiri ya leo.

Mshambuliaji huyo aliyenunuliwa kwa ada ya pauni 75 milioni akitokea Everton alifunga bao hilo dakika ya 38 katika mchezo ambao United walitoka nyuma na kuibuka na ushindi huo kufuatia bao la kusawazisha la Henrikh Mkhitaryan baada Luis Silva kufunga la uongozi kwa upande wa Salt.

Lukaku akifunga bao baada ya kumpiga chenga kipa

United walibadili wachezaji wote 11 kipindi cha pili huku beki Antonio Valencia akionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na kiungo Juan Mata akitolewa nje kwa kuumia enka.

Kuumia kwa Mata na kadi nyekundu ya Valencia kuliwafanya United kushindwa kucheza vizuri ukilinganisha na mchezo wa kwanza wa maandalizi dhidi ya LA Galaxy walioibuka na ushindi  mnono wa mabao 5-2.

Victor Lindelof na Phil Jones walianza kama mabeki wa kati huku Lukaku akianza katika mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge kutoka Everton.

Mshambuliaji Jesse Lingard alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo licha ya kutofunga bao.

 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *