Kimataifa

Ureno, Mexico Zatinga Nusu Fainali Mabara

on

MOSCOW, Urusi
TIMU za Ureno na Mexico zimetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mabara baada ya kushinda michezo yao ya mwisho ya kundi A.

Ureno iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya New Zealand wakati Mexico wakiwafunga wenyeji Urusi mabao 2-1. Mechi zote zilichezwa muda mmoja ili kuepuka kupanga matokeo.

Mexico wakishangilia ushindi wao dhidi ya Russia

Mabao ya Ureno yalifungwa na Cristiano Ronaldo kwa mkwaju wa penalti, Bernardo Silva, Adrien Silva na Luis Nani wakati yale Mexico yalifungwa na Hirving Lozano na Nestor Araujo huku lile Urusi likifungwa na Aleksandr Samed.

Ureno imemaliza kinara wa kundi hilo ikiwa na pointi saba sawa na Mexico lakini wakiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.

Kesho kutakuwa na michezo ya mwisho ya kundi B ambapo Ujerumani itacheza dhidi ya Cameroon huku Chile akicheza na Australia.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *