Kimataifa

Ureno Yaambulia Nafasi ya Tatu Mabara

on

MOSCOW, Ureno
URENO imekuwa mshindi wa tatu wa michuano ya kombe la mabara baada ya kuifunga Mexico mabao 2-1 katika muda wa nyongeza baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mechi ya kumtafuta mshindi watatu.

Mexico walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya beki Luis Neto kujifunga dakika ya 54 katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Javier Hernandez ‘Chicharito’ kabla ya Pepe kusawazisha dakika ya 90 akimalizia krosi ya Ricardo Quaresma.

Adrien Silver aliifungia Ureno bao la ushindi kwa mkwaju wa penati dakika ya 104 na kuifanya Mexico kufungwa mabao 10 na kuwa ndiyo timu iliyofungwa mabao mengi zaidi katika michuano hiyo hadi sasa.

Wachezaji Nelson Semedo wa Ureno na Raul Jimenez wa Mexico walitolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na mchezo usio wa kiungwana.

Mchezo wa fainali utapigwa saa 3 usiku ambapo Ujerumani itacheza dhidi ya Chile katika mechi inayotarajiwa kuwa kali kutokana uimara wa timu zote.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *