Kimataifa

Urusi Watamba Nyumbani Kombe la Mabara

on

MOSCOW, Urusi
WENYEJI wa michuano ya komne la mabara timu ya taifa ya Urusi imeanza vyema mashindano hayo baada ya kuifunga New Zealand mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi.

Mchezo huo uliohudhuriwa pia na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin pamoja na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) Giann Infantino ulikuwa wa upande mmoja huku wenyeji wakionekana kutawala kila idara.

Mabao hayo ya wenyeji yalifungwa na Michael Boxall dakika ya 31 kabla ya Fedor Smolov kuongeza la pili dakika ya 69 na kuwafanya wenyeji kuondoka na pointi zote tatu.

Mlinda mlango wa New Zealand Stefan Marinovic alifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo ya wachezaji wa Urusi ambao muda mwingi wa mchezo walikuwa langoni mwake.

Mchezo mwingine wa kundi A utapigwa kesho kati ya Mexico dhidi ya Ureno huku Cameroon na Chile wakikutana katika mechi ya kwanza ya kundi B.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *