Boiplus TV

+VIDEO: Kapombe Aizungumzia Jezi Yake Namba 15 Simba

on

BEKI mpya wa timu ya Simba Shomari Kapombe aliyesajiliwa akitokea Azam FC amesema hatamvua jezi namba 15 Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ licha ya kwamba alikuwa akiitumia miaka ya nyuma akiwa na Wekundu hao.

Kapombe ambaye amerejea kwa mara ya pili katika timu ya Simba alikuwa akivaa jezi namba 15 ambayo kwasasa inavaliwa na Zimbwe aliyejiunga na Wekundu hao akitokea Kagera Sugar na kugeuka kuwa mchezaji muhimu huku msimu uliopita akichaguliwa mchezaji bora wa ligi.

Beki huyo wa kulia ameiambia BOIPLUS kuwa atavaa jezi nyingine yoyote atakayopewa na viongozi wake na sio lazima kutumia namba 15 kwasababu tu alikuwa akiivaa hapo mwanzo.

“Siwezi kuizungumzia jezi namba 15 kwavile nilishaiacha na mtu aliyekuwa akiivaa ameifanyia kazi nzuri kwahiyo siwezi kumfuata anipatie.

“Nitasubiri viongozi watanipa jezi gani basi nitaivaa, kikubwa mimi naenda pale kufanya kazi, siendi kuchagua namba,” alisema Kapombe.

Wakati yupo Azam Kapombe alikuwa akivaa jezi namba 4 ambayo kwa Simba inavaliwa na kiungo Mohammed Ibrahim.

Shomari Kapombe (kushoto) akiwa na jezi namba 15 wakati akiitumikia Simba

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *