Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

+VIDEO: Kisa kuifunga Yanga, mama aibua khanga iliyonunuliwa 1973

Alinunuliwa na mama yake kama zawadi

0 982

Ushabiki wa Simba na Yanga ulipungua nguvu ila sasa naona umeanza kurudi ndio sababu nimeitoa khanga yangu sandukuni

MAMA mmoja anayefahamika kwa jina la Zena Shaaban Salmin (57) mkazi wa jiji la Mbeya amewashtua wadau wa soka hasa mashabiki wa Simba baada ya kutoa sandukuni khanga iliyonunuliwa 1973 tena ikiwa katika hali nzuri kama mpya kabisa.

Mama huyo mkazi wa mtaa wa Isanga alitoa khanga hiyo baada ya kufurahishwa na ushindi wa bao 1-0 walioupata Simba dhidi ya Yanga siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.

Akizungumza na mwakilishi wa BOIPLUS jijini Mbeya, mama huyo alisema alinunuliwa khanga hiyo na mama yake mzazi baada ya Simba kuibuka mabingwa ambapo alikuwa akikitumia kipande kimoja huku kingine akikihifadhi sandukuni kabla ya kukiibua hapo jana.

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao pekee katika mchezo huo lililofungwa na Emmanuel Okwi

“Nilikuwa nimeitunza tu lakini niliamua kuitoa baada ya kufurahishwa na matokeo ya Simba dhidi ya Yanga, yalinifanya nikumbuke ushabiki wetu wa miaka hiyo.” Alisema.

Related Posts
1 of 32

Bi. Zena alisema mama yake ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Simba alinunua khanga hizo wakati yeye ana umri wa miaka 13 tu na ndipo mapenzi yake kwa Wekundu hao yalipozidi kushamiri.

Akielezea ushabiki wa enzi hizo Bi. Zena alisema haukuwa wa kiwango cha chini kama sasa kwani wao walikuwa wakishangilia kwa kuzunguka mtaani huku wakiimba na kucheza mbele wakitanguliwa na mbuzi aliyepambwa kwa nguo nyekundu.

Bi. Zena akiwa na khanga yake

Hata hivyo mama huyo amekiri kuishabikia pia Mbeya City kwavile ni timu ya nyumbani kwao lakini hakuona ‘noma’ kukiri kuwa Simba ndilo chama lake la ‘kumoyo’.

“Simba ndio ya moyoni, hii Mbeya City naishabikia kwavile ni ya nyumbani lakini siku zikikutana mimi nabakia Msimbazi,” alisema mama huyo kwa kujiamini.

Mwisho Bi. Zena aliwataka wachezaji wa Simba kutobweteka kwa kuifunga Yanga kwani bado hawajawa mabingwa na lolote linaweza kutokea hivyo wanapaswa kuendelea kuzifunga timu zote zilizobakia.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...