Kitaifa

+VIDEO: Okwi Rasmi Simba, Kutua Nchini Jumamosi

on

BAADA ya sarakasi nyingi hatimaye kitendawili kimeteguliwa na sasa ni rasmi mshambuliaji Emmanuel Okwi atajiunga na Simba msimu ujao na Jumamosi hii atatua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

Wiki iliyopita kulikuwa na picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikimunyesha mshambuliaji huyo akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspope katika hotel moja nchini Uganda kitu kilichoongeza uvumi wa nyota huyo kurejea kwa Wekundu hao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Hanspope alisema wameamua kumrejesha Okwi Simba kwasababu wamemfuatilia kwa muda mrefu na wanaamini bado ana uwezo wa kuwasaidia katika michuano ya kitaifa na kimataifa.

Hanspope ameshangazwa na baadhi ya watu kuupinga usajili wa raia huyo wa Uganda kwamba hautakuwa na tija ndani ya kikosi kwa madai ubora wake umepungua na kusema hata katika muda mfupi alioitumikia Sports Club Villa bado aliweza kufunga mabao saba.

“Okwi atatua nchini Jumamosi na atasaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Simba. Uongozi unaamini kuwa usajili wake utakuwa mzuri na msaada mkubwa kwa timu,” alisema Hanspope.

Simba imedhamiria kufanya makubwa msimu ujao kutokana na aina ya wachezaji inaowasajili ambapo tayari wamefanikiwa kuipata saini ya kiungo Haruna Niyonzima kutoka Yanga.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *