Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

+VIDEO: Simba Watua Dar Kimya Kimya, Kocha Agoma Kuzungumza

0 864

KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi Simba kimetua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere majira ya saa 7:25 usiku huu wakitokea nchini Kenya walikoshiriki michuano ya Sportpesa Super Cup na kuibuka washindi wa pili.

Viongozi wa klabu hiyo wakiongozwa na kaimu Rais Salim Abdallah ‘Try Again’ na Haji Manara walikuwa wa kwanza kutoka ambapo haraka waliingia kwenye magari yao na kuondoka huku wachezaji wakitoka mmoja mmoja wakiingia kwenye basi lao dogo bila kuzungumza chochote.

Kocha Masoud Djuma alitoka mwishoni ambapo alipofuatwa na mwandishi wa BOIPLUS ili aweze kuzungumzia mchezo wa fainali pamoja na michuano hiyo kwa ujumla alisema amechoka sana na anahitaji kupumzika huku akitoa ahadi ya kumpigia simu mwandishi huyo kesho.

Related Posts
1 of 35

“Nimechoka sana, naomba uniache nikapumzike kwanza tafadhali, kesho mimi ndiye nitakutafuta tuzungumze. Sijawahi kukataa kuzungumza nanyi lakini leo mtanisamehe,” alisema Masoud.

Simba imeshika nafasi ya pili baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 toka kwa Gor Mahia jioni ya jana na kuwaacha wenyeji hao wakijitwalia tiketi ya kwenda kucheza na Everton kwenye uwanja wa Godson Park nchini Uingereza.

 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...