Kitaifa

+VIDEO: Tazama goli bora la Liverpool kwa miaka 25

on

BAKORA kali ya Steven Gerrard dhidi ya Middlesbrough 2005 imetwaa tuzo ya goli bora la klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita.

Kwa majuma matano mashabiki wa majogoo hao wa Anfield walikuwa wakipiga kura kuchagua goli moja bora zaidi kati ya 1,601 yaliyotingisha kwa miaka 25 kabla washindi watano kutinga fainali.

Steven Gerrard

Mabao ya kukumbukwa ya Robbie Fowler, John Arne Riise, Gerrard, Fernando Torres na Emre Can yalifanikiwa kutinga fainali na mashabiki hao wakaamua kwa kura zao kulichagua moja lililo bora zaidi.

Hatimaye shujaa wa Liverpool Gerrard akafanikiwa kutwaa tuzo hiyo kwa kujizolea asilimia 42 ya kura zote zilizopigwa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *