Kitaifa

+VIDEO: TFF yakana kutoa taarifa yoyote kuhusu Zanzibar

on

AFISA Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Alfred Lucas amesisitiza kuupuzwa kwa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ushiriki wa klabu kutoka Zanzibar kwenye michuano ya Afrika kufuatia kufutwa uanachama na CAF hapo jana.

Asubuhi ya leo kumekuwa na taarifa zilizosambaa mitandaoni zikimnukuu ofisa huyo kuwa kuanzia mwakani bingwa wa ligi kuu ya Vodacom ataiwakilisha nchi katika michuano ya klabu bingwa Afrika wakati bingwa kutoka visiwani Zanzibar akishiriki kombe la shirikisho Afrika.

Akizungumza na BOIPLUS ONLINE TV, akiwa njiani kutoka nchini Rwanda, Lucas amesema taarifa hizo sio za kweli kwakua hazikutoka ndani ya Shirikisho hilo kwa kaimu Rais Wallace Karia, Kaimu Katibu mkuu Salum Madadi wala yeye ambaye anahusika na kitengo cha Habari.

“Taarifa zinazosambaa mitandaoni sio za kweli, hazikutoka TFF ni uzushi mtupu ambao hauna mantiki yoyote. Nawaomba wadau wote wa soka nchini kupuuza uzushi huo,” alisema Lucas.

Lucas amesema pia uzushi huo umempa somo kuangalia jinsi ya kutoa taarifa kutoka ndani Shirikisho hilo ili kudhibiti watu kutunga taarifa wakisingizia TFF na kusababisha usumbufu.

Taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ilikuwa ikimaanisha kuwa klabu ya Simba ingepokwa haki ya kushiriki kombe la shirikisho.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *