Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Vincent Barnabas Aamua Kuwafuata akina Mexime

0 196

WINGA wa Mtibwa Sugar Vincent Barnabas ameamua kujikita kwenye ukocha baada ya wiki iliyopita kutangaza kustaafu soka akifuata nyayo za nyota wengine wa Mtibwa kama Mecky Mexime na Zubeiry Katwila.

Nyota huyo aliyewahi kuitumikia pia klabu ya Yanga, Jumamosi iliyopita alitangazaa kustaafu kucheza soka kabla Mtibwa haijashuka dimbani kupambana na Singida United katika fainali ya kombe la shirikisho la Azam Sports (ASFC) ambao walishinda mabao 3-2 na kutwaa u bingwa huo..

Related Posts
1 of 32

Mkongwe huyo aliyehitimu kozi ya awali ya ukocha hivi karibuni anatarajia kusomea kozi za juu zaidi huku akiweka wazi kuwa malengo yake ni kuhakikisha anapata mafanikio ya juu katika tasnia hiyo kama ambavyo alfanikiwa katika kusakata kabumbu.

“Nina mpango wa kuzidi kujiendeleza kielimu ili nije kupata mafanikio makubwa kwenye ukocha kama ambavyo nimefanikiwa kwenye uchezaji,” alisema.

Mkurugenzi wa Mtibwa, Jamal Bayser alimkabidhi tuzo maalum ya heshima mchezaji huyo katika siku aliyostaafu soka huku akiahidi kumpa nafasi zaidi katika kikosi hicho ambapo kwasasa amepewa jukumu la kukinoa kikosi cha vijana.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...