The sports Hub

Vituo na Makundi Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2019

0 530

LIGI ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itachezwa katika vituo vinne vitakavyokuwa kwenye mikoa ya Tanzania Bara,
ikianza Machi 27, 2019 na kumalizika April 11, 2019 katika hatua ya Makundi.

Timu mbili za juu kutoka katika kila kundi zitafuzu kucheza hatua ya Nane Bora
itakayochezwa kwenye kituo kimoja kitakachotangazwa na TFF.

Hatua nane Bora itakua na makundi mawili yenye timu nne kila kundi, ambapo
timu mbili za juu zitafuzu hatua ya Nusu Fainali na hatimaye Fainali.

Washindi watatu watapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili msimu wa 2019-20.

Vituo vya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) 2019 ni:

  1. SIMIYU – Uwanja wa Halmashauri Bariadi
  2. KATAVI – Uwanja wa Azimio Mpanda
  3. SONGWE – Uwanja wa Vwawa Mbozi
  4. DODOMA – Uwanja wa Mgambo Mpwapwa

KUNDI A – SIMIYU:
Bariadi United (Simiyu), Copco Veteran (Mwanza), Hawita (Mara), Mbuni FC (Arusha),
Red Star (Manyara), Buyuni FC (Dar es salaam), Ujenzi FC (Shinyanga).

KUNDI B – KATAVI:
Mkurugenzi FC (Katavi), Mpui FC (Rukwa), Sabasaba FC (Tabora), Tallinega FC (Kigoma),
Isanga Rangers (Mbeya), Masumbwe FC (Geita), Umoja Chandimu (Kagera).

KUNDI C – SONGWE:
Mpira Pesa FC (Songwe), Deportivo Mang’ula (Morogoro), Makete United (Njombe),
Coastal Star (Pwani), Nzihi FC (Iringa), Top Boys (Ruvuma), DTB FC (Dar es salaam).

KUNDI D – DODOMA:
Mji Mpwapwa FC(Dodoma), Pan African (Dar es salaam), Stand Misuna (Singida),
Majengo United (Tanga), New Generation (Kilimanjaro), Timberland FC (Lindi),
Tandahimba FC (Mtwara).

Get real time updates directly on you device, subscribe now.