Kitaifa

Vodacom wamwaga vifaa kwa timu za ligi kuu

on

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania ambayo ni

mdhamini mkuu wa ligi kuu imegawa vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya sh 500 milioni kwa timu zote 16 kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa ligi 2017/18.

Vifaa vilivyotolewa ni jezi, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vizuia ugoko, nguo za mazoezi, mabegi ya kusafiria, jezi za waamuzi na vibao vya kufanyia mabadiliko uwanjani ili timu hizo shiriki na bodi ya ligi ziendelee na maandalizi kabla ya kuanza kwa ligi Agosti 26.

Jezi za Yanga msimu huu wa 2017/18

Mkurugenzi wa Idara ya masoko na usambazaji wa Vodacom, Hisham Hendi amesema wamegawa vifaa vya michezo kwa timu zote shiriki kama mkataba unavyoelekeza.

“Tunayo furaha kugawa vifaa vya michezo kwa timu shiriki za ligi kwa mujibu wa mkataba tuliosaini, tuna imani ligi ya msimu huu itakuwa ngumu kutokana na maandalizi yanayofanywa na timu zote,” alisema Hendi.

Jezi za Simba msimu wa 2017/18

Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya ligi Boniface Wambura amezitaka klabu kutumia nembo ya mdhamini mkuu kama ilivyoelekezwa ili kutokiuka masharti na kuadhibiwa.

“Nataka nizikumbushe klabu kuhakikisha zinafuata makubaliano ya mkataba kwa kutumia vifaa vilivyotolewa,” alisema Wambura.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *