The sports Hub

Wakenya wamalizana na Manyika Peter Jr.

0 64

KLABU ya KCB inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya imekamilisha usajili wa nyota wa Tanzania Manyika Peter Jr. kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akiwa mchezaji huru.

Manyika alikuwa akikitumikia kikosi cha Singida United kabla hajondoka klabuni hapo ukiwa ni mwendelezo wa nyota kadhaa kuwakimbia ‘Walima Alizeti’ hao wanaonekana kutokaa vizuri kiuchumi. (inaendelea chini ya matangazo)

Manyika Peter Jr. akisaini mkataba wa kuitumikia KCB

Mkataba wa Manyika na Singida ulivunjika hivi karibuni baada ya klabu hiyo kushindwa kumlipa stahiki zake kwa mujibu wa mkataba.

Wakenya hao walivutiwa na kiwango cha kipa huyo wa zamani wa Simba alipofanya vizuri kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup iliyofanyika Nakuru mapema mwaka huu akiwa na kikosi cha Singida.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.