Kitaifa

Wallace Karia Ajitosa Kupambana na Bosi Wake Malinzi

on

MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameingia anga za bosi wake Jamal Malinzi baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Shirikisho hilo utakaofanyika mapema mwezi Agosti.

Mchakato wa uchaguzi huo ulianza jana ambapo Rais Malinzi na Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga Iman Madega walichukua fomu za kugombea nafasi ya Rais huku leo wakiongezeka wengine wawili na kufanya wagombea kufika wanne.

Leo Karia na Fredrick Masolwa nao wameungana na viongozi hao katika kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya Shirikisho hilo.

Wallace Karia

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa habari wa Shirikisho hilo Alfred Lucas imesema katika nafasi ya Makamu wa Rais ina wagombea watatu ambao ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura na Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliojitokeza ni 33 ambapo watu 13 watakaopata kura nyingi ndio watakuwa washindi.

Zoezi la kuchukua fomu litafungwa Juni 22 ambapo Uchaguzi umepangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *