The sports Hub

Wambura Kufikishwa Mahakamani Muda Wowote, Atangaza Kuachana na Soka

0 400

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Kabumbu nchini, TFF bwana Michael Richard Wambura ametangaza rasmi kupitia Mwanasheria wake Emmanuel Muga, kuachana moja kwa moja na masuala ya  soka.

Wakati taarifa hiyo ikiendelea kusambaa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema Wambura anatarajia kupandishwa mahakama ya Kisutu muda wowote kuanzia saa tatu asubuhi ya leo, hiyo Ikiwa ni baada ya kuhojiwa ndani ya Makao Makuu ya taasisi hiyo kuanzia usiku wa jana.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.