Kitaifa

Wanasimba waweka udugu pembeni, kuvurugana JK Youth Park leo

on

TIMU za matawi ya Simba Damu Fans (SDF) na Simba Makini zimeamua kuweka udugu pembeni na kutambiana kuonyeshana ubabe katika mchezo wao wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park, Kidongo chekundu leo saa 9 alasiri.

SDF wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) wiki iliyopita huku Makini wakiwa ndiyo mchezo wao wakwanza.

Nahodha wa SDF Jeff Shimwela ameiambia BOIPLUS kuwa kwa maandalizi waliyofanya mpaka sasa na aina ya wachezaji walionao wana uhakika wa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika wachezaji tuko vizuri, mazoezi tulianza juzi Jumatano na tuna uhakika wa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo,” alisema Jeff.

Kwa upande wake kocha wa Simba Makini, Dizo One alisema wanaiheshimu SDF kutokana na kuwa na wachezaji waliokaa pamoja muda mrefu tofauti na wao ila haiwakatishi tamaa ya kushinda mchezo huo.

“Hii ni mechi yetu ya kwanza, wenzetu wako pamoja muda mrefu ila haitutishi na kusema tutashindwa mchezo huu. Tumefanya mazoezi kwa wiki mbili, wachezaji wana morali ya kushinda mchezo japokuwa tunawaheshimu sana SDF ila haiwaepushi na kipigo,” alisema Dizo One.

Timu hizo ni za matawi ya klabu ya Simba ambapo SDF wanapatikana Tabata huku Simba Makini makao makuu yao yakiwa Kijitonyama.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *