The sports Hub

Washambuliaji Stars wapewa somo

0 24

MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), Peter Tino amewataka washambuliaji wa timu hiyo kuacha uoga wanapokuwa na mpira na badala yake wapambane kupeleka mashambulizi katika lango la Uganda ‘Cranes’ leo katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Misri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mkongwe huyo ndiye straika aliyefunga bao la kuipeleka Taifa Stars katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizochezwa mwaka 1980 huko Lagos, Nigeria alida washambuliaji wa Stars wanauwezo na vipaji vya kufanya vizuri na kuweka historia kama waliyoiweka kikosi chao kwa kuifunga Zambia.

“Mchezaji kama Samatta (Mbwana), Ulimwengu (Thomas) au Simon (Msuva) wanaweza kabisa kutupa matokeo mazuri tunayoyahitaji katika mechi yetu na Uganda wanaweza kupambana kama nilivyojiamini mimi baada ya nahodha (Leodegar Tenga) na wenzangu waliponituma kwenda mbele bila woga na kufunga bao ambalo limeweka rekodi hadi sasa,” alisema Tino.

Aliongeza kuwa anakiamini kikosi cha Stars kinaweza kutimiza ndoto za mashabiki na wadau wa soka ambazo zinasubiriwa kwa kipindi kirefu huku akiwaomba mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia stars.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.