Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Watoto wa Simba, Yanga Kuongoza Mbio za Kuwania Mamilioni ya Azam

0 401

TIMU za vijana za chini ya miaka 20 (U20) za Simba na Yanga zinatarajia kuwaongoza ‘makinda’ wenzao katika michuano ya vijana chini ya umri huo (Uhai Cup) ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi jijini Dodoma.

Timu hizo sambamba na vikosi vya pili vya timu nyingine 14 ambazo zilishiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 zitavaana katika michuano ambayo ratiba yake ilipangwa jana Alhamisi na kugawanywa katika makundi manne ikitarajiwa kuunguruma katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kuanzia Juni 9 hadi 21.

Akizungumza na waandishi wa habari katika upangaji wa makundi hayo, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo amesema kwamba maandalizi yote kwa ajili ya kombe hilo yapo tayari huku baadhi ya maafisa wa shirikisho hilo sambamba na waamuzi wakiwa tayari wameenda Dodoma.

Clifford Ndimbo

“Kila kitu kipo tayari kuelekea mashindano haya ya Uhai Cup ambayo yatafanyika katika kituo kimoja tu kwa msimu huu ambacho ni Dodoma katika Uwanja wa UDOM. Kila kitu kipo katika mpangilio ambapo timu na viongozi tayari wameanza kwenda Dodoma, tumefanya kituo kimoja kutokana na ratiba kubana sana,” alisema Ndimbo.

Related Posts
1 of 32

Afisa Masoko wa TFF, Aron Nyanda amesema kwamba wanawakaribisha wadhamini zaidi kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mashindano hayo ambayo bingwa wake atapata kitita cha shilingi milioni tano.

Aaron Nyanda

“Tunawaomba wadhamini wengine waje kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ligi hii kwa sababu gharama za kuendesha zipo juu sana.¬†Bingwa wa kombe hili atazawadiwa kiasi cha milioni tano, mshindi wa pili milioni tatu na wa tatu milioni moja, pia kuna zawadi kwa mfungaji na kocha bora na timu yenye nidhamu ,” alisema Nyanda.

Makundi ya kombe hilo ni haya hapa chini;

 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...